Wanaopata fursa ya kusoma nje ya nchi wafundwa

0
196

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa  Joyce Ndalichako amewataka vijana wanaopata fursa ya kusoma nje ya nchi, kuzingatia masomo yao, ili  waweze kupata ujuzi utakaoiwezesha Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako ametoa wito huo jijini Dar es salaam, wakati wa hafla ya kuwaaga Wanafunzi wa Kitanzania waliopata nafasi ya kwenda kusoma nchini China.

Waziri huyo wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, pia ameishukuru Serikali ya China kwa kukubali ombi la Rais John Magufuli  la kusomesha Wataalamu wa afya wa hapa nchini kila mwaka nchini China.

Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini, – Wang Ke amesema kuwa China itaendelea kutoa nafasi za masomo nchini humo kwa Watanzania ili kuendeleza uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.