Luiz Asema Arsenal ni Timu Sahihi Kwake Kwa Sasa

0
144

Mlinzi wa zamani wa timu ya Chelsea ya nchini England, -David Luiz amesema kuwa malengo na kutaka kutimiza ndoto zake ndio sababu kubwa iliyomfanya ajiunge na timu ya Arsenal na kwamba kubaki kwenye timu ya Chelsea lingewakuwa ni jambo gumu kwake maishani.

Mlinzi huyo raia wa Brazil mwenye umriwamiaka32, Jumamosi iliyopita alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na Arsenal na kupata ushindi wa bao mbili kwa moja dhidi ya Burnley tangu aondoke Magharibi mwa jiji la London na kwenda Kaskazini mwa jiji hilo.

Luiz mwenye mbwembwe nyingi amesema kuwa, yeye siku zote ni mtu mwenye malengo na ndio maana akaamua kuachana na Chelsea na siku zote amekuwa mtu mwenye kutaka kupata changamoto mpya na vitu vipya kwenye maisha yake.

Habari zaidi zinasema kuwa, kocha mpya wa Chelsea, – Frank Lampard alimueleza Luiz kuwa hana nafasi yakudumukwenyekikosichake, kauliiliyomkasirishanakuamuakuondokanakwenda kujiunga na Arsenal.

Mwenyewe Luiz amekaririwa akisema kuwa, kila mtu anafahamu kama alikua ni mwenye furaha akiwa Chelsea na kushinda mataji mengi,  lakini baada ya kufanya majadiliano na kocha mpya Frank Lampard na kumjulisha mipango yake, aliona kuwa ni tofauti na alivyotaka, hivyo akaona ni vema aondoke.