China Yapeleka Wanajeshi Katika Mpaka wa Jimbo la Hong Kong

0
406

Askari wa jeshi la China wameonekana wakifanya mazoezi ya kijeshi katika eneo la mpaka wa jimbo la Hong Kong na nchi hiyo, ikiwa ni katika hali ya kujiandaa kwa usalama.

Serikali ya China imeamua kuimarisha ulinzi baada ya maandamano ya kupinga serikali ya nchi hiyo kuongezeka katika jimbo la Hong Kong yanayoambatana na vitendo vya ghasia ambavyo serikali ya nchi hiyo inasema kuwa sasa vimezidi na kuwa sawa na vitendo vya kigaidi.

Kwa muda uwanja wa ndege wa Hong Kong ulilazimika kufungwa, baada ya waandamanaji kuingia uwanjani hapo na kutatiza safari za ndege huku watu wawili kutoka bara la China wakiwa wamepigwa na waandamanaji uwanjani hapo.