Matumaini ya Kupatikana Dawa ya Ebola

0
221
Diagnosis - Ebola Virus.

Wataalamu wa Afya kutoka taasisi ya NIAID ya nchini Marekani wamesema Ugonjwa wa Ebola   unaweza kuzuilika na kutibika baada ya baadhi ya dawa za aina mbili  kuonesha matokeo mazuri kwa baadhi ya wagonjwa wa Ebola waliotumia dawa hizo.

Akizungumzia hatua hiyo, mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Anthony Fauci, amesema idadi kubwa ya wagonjwa wa Ebola waliotumia dawa hizo, afya zao zimeonekana kuzidi kuimarika na kutoa tumaini la kupatikana kwa kinga na tiba ya ugonjwa huo ambao umesababisha vifo vya mamia ya watu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Dkt. Anthony Fauci

Ameongeza kuwa utafiti wa dawa hizo ulianza kufanyika mwezi Novemba mwaka 2018 chini ya Uratibu wa Shirika la Afya Duniani WHO ambapo Wizara ya afya huko DRC imesema  dawa hizo sasa zitaendelea kusambazwa kwa wagonjwa wengine wa Ebola ili kuendeleza jitihada za kuokoa maisha ya wagonjwa hao.Hata hivyo watafiti wa dawa hizo wameongeza kuwa Dawa hizo zinaweza kuwa na matokeo mazuri zaidi kwa wagonjwa wa Ebola watakaoanza kupata matibabu mapema zaidi.