Spika Pelosi Amshutumu Rais Trump kwa Ubaguzi

0
300

Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi amemshutumu Rais Donald Trump wa Marekani, kwa kuendelea kutoa ujumbe  wa ubaguzi wa rangi dhidi ya wabunge wa chama cha Upinzani cha Democrat wenye asili ya Afrika.

Pelosi ametoa shutuma hizo baada ya rais huyo wa marekani kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuandika maneno ya kashfa yenye viashiria vya ubaguzi wa rangi  dhidi ya mbunge Elijah Cummings wa Maryland aliyepinga mapendekezo ya Trump katika kushughulikia suala la wahamiaji wanaohifadhiwa katika makambi maalumu katika mpaka wa Marekani na Mexico.

Spika huyo amesema matamshi na matendo yanayoashiria ubaguzi wa rangi, havipaswi kuendelezwa kwa kuwa vinaweza kuvuruga umoja na amani nchini humo kwa kuwa na jamii yenye matabaka.