Kesi Ya Viongozi wa CHADEMA Yasogezwa Mbele

0
595

Mahakama wa Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha hadi mwezi Agosti mwaka huu kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi Tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA akiwemo mwenyekiti wake Freeman Mbowe kutokana na ushahidi upande wa jamhuri kutokamilika.

Akitoa tamko hilo Jijini Dsm Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba amesema kesi hiyo imechukua muda mrefu na hivyo kuamua kusikilizwa kuanzia Agosti 5, 6 na 7 mfululizo mwaka huu ili hukumu kupatikana.

Mawakili upande wa serikali waliongozwa na Wakili Faraja Nchimbi kutokamilika kutokana na kukosa vifaa vya kusapoti video ya Koplo Charles kama waya chaja na projector ya kuonesha video hiyo.

Mnamo Februari 16 mwaka 2018, katika barabara ya Kawawa Kinondoni-Mkwajuni Mbowe na wenzake 12 ambao hawakuwepo mahakamani wanadaiwa walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika ambako kugoma huko kulisababisha hofu na hatimaye kifo cha Akwilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili.