Malaria Sugu Yaripotiwa Bara la Asia

0
240

Wadudu wa ugonjwa wa malaria waoripotiwa kuwa wagumu kuuawa kwa dawa muhimu za ugonjwa huo,wameanza kuenea kwa kasi katika maeneo ya mbalimbali ya Kusini mashariki mwa bara la Asia.

Hayo yamebainika baada ya watafiti wa masuala ya afya kutoka Uingereza na Thailand kufanya utafiti wa kina ulioonesha ongezeko la wadudu hao sugu wa malaria  wanaoenezwa na mbu kugundulika huko Cambodia, Thailand, Vietnam  na Laos.

Watafiti hao wamesema zaidi ya nusu ya wagonjwa waliotumia dawa chaguo la kwanza, huko Thailand na Vietnam hawakupona baada ya kugundulika kuwa na malaria hiyo sugu.

Hata hivyo watafiti hao wameonya kuwa mbu wanaoeneza wadudu hao  sugu wa malaria huenda wakasambaa na kufikia maeneo mbalimbali ya bara la Afrika ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likiathiriwa na ugonjwa huo na kusababisha vifo, ikiwemo kwa mama wajawazito na watoto wa chini ya umri wa miaka mitano.