Watu zaidi ya Milioni moja wahitaji Msaada Cameroon

0
224

Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu Milioni Moja Nukta Tatu wanahitaji msaada wa kibinadamu katika maeneo mbalimbali nchini Cameroon.

Katika taarifa yake, Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu Elfu Moja na Mia Tatu hawajulikani walipo baada ya kutokea kwa mashambulio nchini Cameroon wiki iliyopita, mashambulio ambayo pia yamesababisha vifo vya watu kadhaa na baadhi ya nyumba kuchomwa moto.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, – Antonio Guterres imeongeza kuwa, hali ni mbaya zaidi katika eneo la Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi la nchi hiyo,  ambako ukiukwaji wa haki za binadamu umekua ukiendelea.

Cameroon imekumbwa na mapigano tangu mwaka 2016, mapigano yaliyosababisha zaidi ya Watu Laki Tano kuyakimbia makazi yao.Mapigano hayo yamekua yakifanywa na Waasi waliopo kwenye  mji wa Bamenda, ambapo wanataka kujitenga kwa mji huo.