Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa MZEE MKONGEA ALLY amewataka wananchi katika Manispaa ya Wialaya ya Temeke kutunza na kuilinda miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli wilayani humo ili miradi hiyo iweze kuwasaidia kujikwamua katika changamoto za umaskini.
Akizungumza mara baada ya kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo,Mkongea amesema kufunguliwa kwa miradi hiyo kutawasaidia wananchi kuondokana na kero mbalimbali.