Mwinyi aeleza kutofurahishwa na January kutumia Picha yake

0
157

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi ameelezea kutofurahishwa na kitendo kilichofanywa na aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba kutumia picha yake katika mitandao ya kijamii muda mfupi baada uteuzi wake kutenguliwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza nyumbani kwake jijini Dsm, Mzee Mwinyi amesema picha iliyotumiwa na January Makamba katika mitandao ya kijamii ikimuonesha wamekti pamoja wakicheka muda mfupi baada ya kutenguliwa uwaziri imemkwaza kutokana kutumiwa katika mazingira na wakati usiostahili.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi anazungumzia pamoja na mambo mengine picha yake ambayo imeonekana kwenye mitandano ya kijamii mwishoni mwa wiki akionesha kufurajia jambo.

Akizungumzia picha hiyo inayomuonesha akifurahia jambo na aliyekuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais Muungano na Mazingira January Makamba, Mzee Mwinyi amesema hakufurahishwa na namna picha hiyo ilivyotumika.

Kuhusu waraka ulioandikwa na Makatibu Wakuu Wastaafu Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba kwenda kwa Baraza la Viongozi Wastaafu, Mzee Mwinyi amesema huo ni Utoto.

Mzee Mwinyi amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli kwa juhudi anazozifanya kuleta maendeleo.