Marekani Yaitungua Ndege ya Iran

0
521

Marekani  imeitungua na kuiharibu ndege ya Iran isiyokuwa na rubani, iliyoikaribia  moja ya Manowari zake za kivita karibu na njia kuu ya meli za Kimataifa  katika eneo la Hormuz.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa,  hatua hiyo ni ya kujilinda kwa kuwa ndege hiyo ya Iran ilikuwa ikitishia usalama wa Manowari hiyo pamoja na Wafanyakazi wake.

Trump amesema kuwa ndege hiyo imeharibiwa kabisa na kwamba kitendo cha Iran kupeleka ndege hiyo karibu na Manowari yake, ni cha uchokozi.