Instagram yatangaza kuficha idadi ya maoni ya kupenda picha au video “Likes” kutoka kwenye machapisho ili kujaribu “kuondoa shinikizo” kwa watu “remove social media pressure”.
Mabadiliko yameanzishwa katika nchi kadhaa kama sehemu ya majaribio makubwa ya kimataifa na kisha wataamua kama watafanya kwa nchi zote kwa kutoa toleo jipya la kudumu.
Kampuni ya Instagram imesema sasa inataka watu wafatilie picha na video ambazo mtumiaji anazichapisha “post” katika kurasa yake na sio idadi ya maoni ya kupenda picha au video hizo ila kila mtumiaji katika kurasa yake anaweza kuziona kwa kubofya katika idadi ya watu waliopenda bila marafik zake kujua idadi hiyo.
Mwaka 2017, uchunguzi ulibaini kuwa vijana walipiga kura ya Instagram kama mtandao mbaya zaidi wa kijamii hususan katika afya yao ya akili.
Je, unadhani mabadiliko haya yataboresha uzoefu wako wa Instagram?