Watu Ishirini na Sita wamekufa na wengine Arobaini wamejeruhiwa baada ya mtu mmoja kupulizia kimiminika kinachotoa mlipuko katika Studio ya kutengeneza vikaragosi, iliyopo kwenye mji wa Kyoto nchini Japan.
Habari kutoka nchini Japan zinasema kuwa,baada ya mtu huyo kupuliza kimiminika hicho, studio hiyo yenye ghorofa tatu ilianza kuwaka moto.
Polisi katika mji wa Kyoto wamesema kuwa, watu wengine Thelathini hawajulikani walipo kufuatia tukio hilo na jitihada za kuwatafuta zinaendelea.
Tayari mtu anayetuhumiwa kufanya tukio hilo amekamatwa na amelazwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu, baada ya kupata majeraha makubwa.