Watu Kumi wamekufa na wengine wengi wamenasa kwenye vifusi, baada ya jengo moja lenye ghorofa Nne kuanguka katika mji wa Mumbai nchini India.
Hadi sasa, chanzo cha kuanguka kwa jengo hilo hakijafahamika.
Wataalamu wa ujenzi nchini India wamesema kuwa, huenda sababu za kuanguka kwa jengo hilo lililojengwa zaidi ya miaka Mia Moja iliyopita ni mvua kubwa, zinazoendelea kunyesha nchini humo.
Vikosi vya uokoaji katika mji huo wa Mumbai kwa sasa, vinaendelea kuwatafuta watu walionasa kwenye vifusi.
Kufuatia kuanguka kwa jengo hilo lililokua likikaliwa na familia 15, Waziri Mkuu wa India, – Narendra Modi ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliokufa katika tukio hilo.
Matukio ya kuanguka kwa majengo yamekua yakitokea mara kwa mara nchini India, na kusababisha vifo vya takribani watu Elfu Mbili kwa mwaka