Rais Magufuli Afanya Ziara Gereza La Butimba

0
389

Rais Dokta John Magufuli amewaagiza makatibu wakuu wa Wizara ya Uchukuzi, Fedha na Kamishina wa TRA kuhakikisha vifaa vya uundaji meli vinafikishwa jijini Mwanza ifikapo Julai 20 mwaka huu.

Rais ametoa agizo hilo baada ya kuonekana kuwepo kwa ucheleweshwaji wa vifaa ya uundaji wa meli hiyo alipofanya ziara katika bandari ya Mwanza kusini ambapo pia amekagua ukarabati wa Meli mbili za MV VICTORIA na MV BUTIAMA ili kuimarisha miundo mbinu ya usafiri katika Ziwa Victoria.

Mradi wa ukarabati wa Meli hizo ulianza Machi tano mwaka huu ambapo unatarajiwa kukamilika Machi mwaka 2020.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ametembelea Gereza la Butimba Mkoani Mwanza na kuzungumza na wafungwa, mahabusu pamoja na askari magereza ambapo amesema serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Askari Magereza na kuonya tabia baadhi ya askari kuwabambikizia kesi raia.

 Aidha Rais Magufuli ameahidi kupeleka magari kwa ajili ya usafiri wa askari magereza na Wafungwa wa Gereza la Butimba Mwanza pamoja na Trekta kwa ajili ya shughuli za Uzalishaji Mali.