Kisimiri yaongoza matokeo kidato cha sita

0
479

Baraza la Mitihani la Tanzania-NECTA, limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwezi Mei mwaka huu ambapo ufaulu unaonesha kuongezeka ikilinganishwa na mwaka jana.

Akitangaza matokeo hayo mjini Unguja, Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt. Charles Msonde amesema ubora wa ufaulu wa wasichana kwa mwaka 2019 umezidi ule wa wavulana kwa asilimia 1.07.

Ufaulu wa jumla katika mitihani ya kidato cha sita mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 0.74 ambapo mwaka 2018 ufaulu ulikuwa asilimia 97.58 na mwaka huu ni 98.32.

Dkt. Msonde ametaja shule kumi bora kitaifa kuwa ni Kisimiri(Arusha), Feza Boys(Dar Es Salaam), Ahmes(Pwani), Mwandet(Arusha), Tabora Boys(Tabora), Kibaha(Pwani), Feza Girls(Dar Es Salaam) St. Mary’s Mazinde Juu(Tanga), Canossa(Dar Es Salaam) na Kemebos(Kagera).

Aidha shule kumi za mwisho kitaifa ni Nyamunga(Mara), Haile Selassie(Mjini Magharibi), Tumekuja (Mjini Magharibi), Bumangi(Mara), Buturi(Mara), Mpendae(Mjini Magharibi) Eckernford(Tanga), Nsimbo(Katavi), Mombo(Dodoma) na Kiembe Samaki “A” Islamic(Mjini Magharibi)