Rais Dkt. JOHN MAGUFULI aagiza kuchukuliwa hatua kwa watumishi wanaojihusisha na ujangili

0
337

Rais Dkt. JOHN MAGUFULI amezindua Hifadhi ya Taifa ya BURIGI wilayani CHATO mkoani GEITA na kumuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. HAMISI KIGWANGALA kuwachukulia hatua za kisheria watumishi ambao si waadilifu wanaotaka kuhujumu rasilimali za Taifa.

Akizindua hifadhi hiyo Rais Dkt. MAGUFULI amesema watumishi hao wamekuwa wakishirikiana na majangili ambao wanawaua wanyapori katika hifadhi za Taifa.