Marekani kuishutumu Iran

0
407

Marekani imetoa mkanda wa video ambao inadai kumuonyesha mmoja wa askari wa Iran akiondoa kifaa kinachodaiwa kuwa ni mlipuko katika moja ya meli za mafuta katika Ghuba ya Oman.

Taarifa zaidi zinasema Marekani inaamini kuwa video hizo zilizotolewa na wapelezi wake ni za askari wa Iran ambaye alitaka kupoteza ushahidi wa tukio hilo.

Rais Hassan Rouhani wa Iran amekanusha taarifa zinazotolewa na Marekani dhidi ya nchi yake kuhusika na mlipuko katika meli hiyo ya mafuta.

Hatua hiyo ya Marekani kuishutumu Iran inaelezwa huenda ikasababisha kupanda kwa bei ya mafuta na kuzua wasiwasi kuhusu mapambano mapya kati ya Marekani na Iran.