Marekani Yatuma Mjumbe Sudan Kujaribu Kutatua Mgogoro wa Kisiasa

0
296

Mjumbe maalum wa nchi ya Marekani Donald Booth, yuko nchini Sudan akijaribu kutatua mgogoro wa kisiasa uliozuka nchini humo, baada ya kufanyika kwa mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa nchi hiyo Omar Al Bashir.

Booth tayari amekutana na viongozi wa maandamano nchini Sudan, pamoja na mwanadiplomasia mkuu anayeiwakilisha nchi ya Marekani, barani Afrika kwa ajili ya mazungumzo.

Upande wa upinzani nchini Sudan umeendelea kusisitiza kuwa ni lazima jeshi la nchi hiyo kuwajibishwa, kutokana na msako mkali uliofanyika wiki iliyopita dhidi ya waandamanaji wanaopinga serikali na kusababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja.

Watu hao waliuawa na askari wa jeshi la Sudan na wengine miili yao kutoshwa katika mto Nile. Waandamanaji wanaishinikiza serikali ya kijeshi ya Sudan kurejesha utawala wa kiraia.