Mtonga anachukuwa nafasi ya Dkt Omari Nundu ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania.
Uteuzi wa Dkt Nundu katika nafasi hiyo unafuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na kampuni ya Bharti Airtel International juu ya uendeshaji wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania anapaswa kuteuliwa na Serikali ya Tanzania.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Afisa Mkuu wa Ufundi pia anateuliwa na Serikali ya Tanzania, na aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo ni Dkt Prosper Mafole.
Wajumbe wengine watakaoiwakilisha Serikali katika Bodi ya Airtel Tanzania ni John Sausi na Lekinyi Mollel.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, – Ikulu imesema kuwa uteuzi huo unaanza hii leo.