Lugha Rasmi Zinazotumika Katika Mfumo Wa Elimu

0
269

Serikali imesema pamoja na kufanya jitihada mbalimbali za  kuiendeleza lugha ya Kiswahili, bado kuna umuhimu wa kutumika kwa lugha ya Kiingereza kwa maendeleo ya Taifa.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa Bungeni jijini Dodoma na  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na kuongeza kuwa Tanzania ina walimu wa kutosha wa lugha ya Kiswahili na itahakikisha lugha hiyo inakua bila kuathiriwa na lugha ya Kiingereza.