Rais Ibrahim Boubacar Keita Wa Mali Kukatisha Safari

0
329

Rais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali amelazimika kukatisha safari yake nchini Switzerland  ambako alikua akihudhuria mkutano, kufuatia mauaji ya takribani watu mia moja nchini humo.  Serikali ya Mali imesema kuwa mauaji hayo yamefanywa na  vikundi vinavyodhaniwa kuwa ni vya kigaidi, huku taarifa kutoka katika kijiji cha Dogon yalipotokea mauaji hayo zikisema kuwa yametekelezwa na watu wa kabila la Fulani.