Timu zisizo na viwanja kukiona-Karia

0
97

“Hili sio mara ya kwanza kulisema, niliwahi kuliongea huko nyuma. Sasa hivi hatutakubali tena, timu inayoshiriki Ligi Kuu lazima iwe na uwanja wake wa mazoezi,” amesema Rais wa TFF, Wallace Karia, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika Moshi, Kilimanjaro.

Karia ameeleza kuwa umiliki wa uwanja wa mazoezi ni muhimu kwa maendeleo ya soka la nchi. “Uwanja wa kuchezea mechi lazima timu iwe na mkataba wa matumizi, lakini kwa mazoezi tunataka kila timu iwe na hati ya umiliki wa uwanja. Hii ni hatua ya kuhakikisha timu zinajiandaa vizuri na kukuza vipaji.”

Ameongeza kuwa, adhabu kali zitatolewa kwa timu zitakazoshindwa kutimiza masharti hayo. “Huu ni wakati wa kuboresha miundombinu ya soka nchini. Lazima kila klabu ichukulie hili kwa uzito wake ili kuendana na viwango vya kimataifa,” amesema.

Sasa swali kwa mashabiki wa soka ni, ni timu gani ya kwanza itakiona cha mtema kuni kwa kukosa uwanja wa mazoezi inao umililliki? Wakati majibu yakisubiriwa, inaonekana TFF iko makini kuhakikisha soka la Tanzania linapiga hatua.