Wanawake wa jamii za wafugaji wapiga mzigo mradi wa EACOP

0
42

Moja ya faida za mradi wa kimkakati wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga, Tanzania ni kutoa ajira kwa makundi mbalimbali wakiwemo wanawake kufanya kazi hata zilizozoeleka kuwa ni za wanaume, tena katika jamii ambazo wanawake wanachukuliwa kuwa watu wa kukaa nyumbani na kulea watoto.

Mradi huo umeshaajiri Watanzania zaidi ya 7,800 ambao wanafanya kazi za kitaalamu na za zisizo za kitaalamu huku wanawake wakihamasishwa kuzichangamkia.

Darema Alphonce, mmoja wa maofisa uhusiano jamii katika mradi huo, akizungumza katika eneo la Igunga, Tabora, anasema wamefanikiwa kuishawishi jamii ya wafugaji kuruhusu akina mama kufanya kazi kwenye mradi na kuongeza kipato kwenye familia zao.

Darema anashukuru kuwepo kwa mradi huo akikiri kuwa umekuwa msaada mkubwa kwa jamii yao baada ya kuwapa elimu wanaume kuruhusu wanawake kwenye familia zao kufanya kazi mbalimbali ndani ya mradi.

“Wafugaji kikawaida yao, wanawake ni watu wa kukaa nyumbani na kulea watoto, lakini mradi huu umebadilisha mitazamo ya wanaume na kuweza kuwaruhusu wanawake kufanya kazi,” amesema Darema ambaye pia anatoka katika jamii ya Wataturu ambao ni wafugaji.