Meneja wa Yanga, Walter Harrison, amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya shilingi milioni 1 na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa kosa la kuwashurutisha waamuzi waliochezesha mchezo wao dhidi ya Coastal Union kuamini maoni yake. Imeelezwa kwamba hatua yake ya kutumia kompyuta mpakato kuwaonesha marudio ya video ya matukio mbalimbali ya mchezo huo kama ushahidi wa yale aliyokuwa akiyalalamikia, kamati imetafsiri kitendo hicho kama kinachoweza kushawishi shari au vurugu uwanjani.
Walter atakosa mechi dhidi ya Azam itakayochezwa kesho Jumamosi, mchezo na Tabora United utakaochezwa Novemba 7, na mchezo wa Yanga dhidi ya Fountain Gate.