Mradi wa Bomba la Mafuta waendelea kwa kasi

0
32

Ujenzi wa Mradi wa kimkakati wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga, Tanzania umeendelea kushika kasi ambapo sasa ulazaji wa mabomba umeanza.

Awali mradi huo wenye maslahi mapana ya Taifa na Afrika kwa ujumla ulianza kupigiwa kelele kuwa umesimama wakati kazi inaendelea huku ukizalisha ajira nyingi kwa Watanzania wakijipatia pesa na ujuzi mpya kupitia mradi huo.

Asiad Mrutu, mratibu wa mradi huo kwa upande wa Tanzania anasema kazi inaendelea na mradi unazingatia viwango vya kimataifa ikiwepo haki za binadamu, utunzaji wa mazingira na kuchunga haki za wanyama na viumbe hai vyote.

Inaelezwa kuwa mradi huu unatarajiwa kugharimu takribani shilingi trilioni 11 hadi kukamilika kwake, huku bomba lake likiwa na urefu wa kilomita 1,443 kwa ujumla. Kwa upande wa Tanzania pekee, bomba hilo lina urefu wa kilomita 1,147.

@simbeyezekiel