Abiria kwenye treni mchongoko

0
145

Abiria kwenye treni Mchongoko

Baadhi ya abiria wakiwa safarini kuelekea Jijini Dodoma kwa kutumia usafiri wa Treni ya kisasa ya Mchongoko.

Safari ya kwanza ya treni ya kisasa ya Mchongoko imeanza leo Novemba Mosi, 2024 kutoka Stesheni ya Magufuli mkoani Dar es Salaam hadi Stesheni Kuu ya Samia mkoani Dodoma.

Treni Mchongoko ina vichwa mbele na nyuma tofauti na treni zingine zenye kichwa kimoja, huku ikibeba jumla ya abiria 589 na inatembea kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

TBC Digital imefunga safari kufuatilia safari hiyo mwanzo hadi mwisho ambapo utapata taarifa mbalimbali.

✍🏾📸 @clementsilla