Ajali yaua watu 14 Hai

0
557

Watu 14 wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa baada ya basi dogo aina ya Costa walilokuwa wakisafiria kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro kwenda Arusha kugongana na lori la mizigo eneo la Mto Kikafu wilayani Hai.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya mkoa huo Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa watu sita walifariki hapohapo na wengine wanane walifariki dunia walipokuwa wakikimbizwa hospitalini.

Msemaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi, Venna Karia amesema wamepokea majeruhi 11 wa ajali hiyo ambapo watano wamepelekwa katika Hospitali ya Kanda ya KCMC kwa matibabu zaidi.