Bilioni 3.7 zajenga hospitali Madaba

0
353

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi Bilioni 3.7 kujenga majengo 16 katika Hospitali ya Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt. Wambura Chacha amesema hata hivyo hospitali hiyo inahitaji majengo 31 zaidi lakini akasema imeanza kutoa huduma mbalimbali kulingana na hatua ya ujenzi na vifaa tiba vilivyopo.

Amezitaja huduma ambazo zimeanza kutolewa katika hospitali hiyo kuwa ni huduma za afya za wagonjwa wa nje, huduma ya kliniki ya mama, baba na mtoto na huduma ya dharura na kwamba wanasubiri vifaa kutoka serikali kuu ili hospitali hiyo iweze kuanza kutoa huduma za afya zinazilingana na hadhi ya hospitali ya wilaya.