Watuhumiwa wa mauaji ya Asimwe wafikishwa mahakamani

0
352

Watuhumiwa wa mauaji ya mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyekuwa na umri wa miaka miwili na nusu yaliyotokea mkoani Kagera, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba leo Juni 28, 2024.

Mtoto Asimwe alitekwa na watu wasiofahamika Mei 30, 2024 nyumbani kwao katika Kijiji cha Mulamula Wilaya ya Muleba Mkoa wa Kagera na mwili wake ulipatikana Juni 17, 2024 ukiwa umenyofolewa baadhi ya viungo.