Wafanyabiashara wa Mjini Iringa leo wamegoma kufungua maduka yao, hali iliyoleta adha kwa wakazi wa mji huo kutokana na kukosa huduma.
Habari zaidi kutoka mkoani Iringa zinaeleza kuwa maduka mengi katikati ya mji yamefungwa.
Hali hiyo inaelezwa kwenda kinyume na ahadi ya Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Iringa, Kola Mtende aliyesema kuwa wao hawatagoma kufungua biashara zao.