Wauguzi wafundwa kuzingatia haki, usalama

0
261

Wauguzi na wakunga wametakiwa kuzingatia haki, usalama, kutohatarisha uhai na kuheshimu imani, mila na desturi ambazo haziathiri utoaji wa huduma za kiuuguzi na ukunga.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Usajili, Leseni na Maadili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), Jane Mazigo wakati wa utoaji wa mafunzo ya kuhamasisha maadili, sheria ya uuguzi na ukunga pamoja na huduma bora kwa wateja mkoani Tanga.

Mbali na utoaji mafunzo maafisa kutoka TNMC watatembelea vyuo vya uuguzi na ukunga ili kujionea hali halisi ya utoaji wa mafunzo ikiwa ni pamoja na kusisitiza uzingatiaji wa miongozo.