Mfahamu Donald Trump

0
557

Donald John Trum, mfanyabiashara mkubwa na mwanasiasa maarufu ni miongoni mwa watu maarufu ambao leo Juni 14, 2024 wanasherehekea siku zao za kuzaliwa.

Donald Trump ambaye amewahi kuwa Rais wa Taifa kubwa la Marekani kati ya mwaka 2017 na 2002 akiwa Rais wa 45 wa Taifa hilo, leo anatimiza umri wa miaka 78.

Alizaliwa
Juni 14, 1946 huko Queens, New York City akiwa ni mtoto wa nne wa Fred Trump na Mary Anne MacLeod Trump na kukulia katika mtaa wa Jamaica Estates wa Queens.

Akiwa na umri wa miaka 13 aliingia Chuo cha Kijeshi cha New York na mwaka 1964, alijiunga na Chuo Kikuu cha Fordham.

Miaka miwili baadaye, alihamia Shule ya Wharton ya Chuo Kikuu cha Pennsylvania, na kuhitimu Mei 1968 Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika uchumi.

Mwenyewe anasema hajawahi kunywa pombe, kuvuta sigara wala kutumia dawa za kulevya.

Mwaka 1977, Trump alifunga ndoa na mwanamitindo wa Ivana Zelníčková na kubahatika kupata watoto watatu, lakini hata hivyo wenzi hao walitalikiana mwaka 1990, kufuatia uhusiano wa Trump na mwigizaji Marla Maples ambao walioana mwaka wa 1993 na kutalikiana mwaka wa 1999.

Katika harakati za siasa Donald Trump alishinda uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 kupitia Chama cha Republican.