Saratani bado tishio

0
279

Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyopo mkoani Dar es Salaam, Frank Ruta amesema bado kuna umuhimu kwa jamii kupatiwa elimu zaidi ya uelewa kuhusu ugonjwa wa saratani ambao umekuwa ukisababisha vifo vya watu wengi nchini.

Akizumgumza wakati wa mjadala wa mapambano dhidi ya Saratani Dkt.Frank amesema ugonjwa huo unazidi kuwa tishio nchini kutokana na takwimu kuonyesha wagonjwa wanaongezeka siku hadi siku.

Dkt. Frank ameishauri jamii kuwa na tabia ya kupima afya mara kwa mara kujua kama wana ugonjwa wa saratani ama la, ikiwa ni sehemu ya mapambano ya ugonjwa huo unaoonekana kuwa bado tishio hasa kwa wanawake.