Hoja zijibiwe kabla ya Juni 30

0
182

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Buriani amesema kati ya halmashauri 11 za mkoa huo, 10 zimepata hati safi isipokuwa moja ya Kilindi.

Hata hivyo amesema licha ya halmashauri hizo kupata hati safi, bado utekelezaji wa mapendekezo ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hauridhishi kwa kuwa hoja nyingi bado hazijapatiwa ufumbuzi.

Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo wilayani Mkinga alipoongoza kikao cha Baraza maalumu la hoja za ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/ 2023.

” Jumla ya hoja 72 zilizotolewa katika hesabu za CAG kwa mwaka 2022/2023 zikijumuisha hoja za nyuma ni hoja 32 pekee zimejibiwa na kufungwa huku hoja 40 sawa na asilimia 60 hazijabiwa”.amesema Dkt. Batilda

Kufuatia hali hiyo, Dkt. Batilda ameziagiza halmashauri ambazo bado hoja zao hazijapatiwa majibu, kushughulikiwa na kupatiwa majibu kabla ya Juni 30, 2024.