Mwanakwaya adakwa akidaiwa kudhalilisha

0
252

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mwanakwaya mmoja wa Parokia ya Mshindo ya Kanisa Katoliki mjini Iringa kwa tuhuma za kumdhalilisha kijana wa miaka 14 ambaye alimwajiri kumuuzia duka lake.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa, Alfred Mbena amesema mtuhumiwa huyo Blass Nicholaus maarufu kama Matowa mkazi wa mtaa wa Kitasengwa mjini Iringa amefanya tukio hilo Juni 9, 2024 majira ya usiku.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda Mbena, siku ya tukio mwanakwaya huyo alirejea usiku na kugonga mlango wa chumba anacholala mfanyakazi wake wa dukani na kumlazimisha kulala nae chumbani kitandani na kisha kumfanyia unyama huo.

Mtuhumiwa alimsababishia kijana huyo maumivu sehemu za siri na hivyo kuamua kumueleza mama yale mlezi ambaye ndiye alitoa taarifa kwa uongozi wa mtaa na kumkamata mtuhumiwa.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na atafikishwa mahaamani mara upelelezi utakapokamilika.