Matokeo ya awali ya Bunge la Ulaya yanaonesha muungano wa Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz umeshindwa ambapo vyama vyote vitatu katika serikali yake vimekuwa nyuma ya vile vya kihafidhina na mrengo mkali wa kulia.
Matokeo hayo yanaibua wito kutoka kwa vyama vya upinzani vya Christian Democratic Union (CDU) na Christian Social Union (CSU) viliyoshinda kwa Scholz vya mrengo wa kati kubadili mkondo au kuandaa uelekeo kwa uchaguzi mpya.
Upinzani unaongeza shinikizo ikiwa ni miezi michache kabla ya uchaguzi muhimu wa kikanda katika majimbo kadhaa ya mashariki ambapo chama cha mrengo wa kulia kinatabiriwa kuibuka na ushindi.
Chanzo: DW