Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema ameamua kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi baada ya chama chake kushindwa vibaya katika uchaguzi wa Bunge la Ulaya.
Akilihutubia taifa kutoka katika makazi ya Rais ya Élysée jijini Paris, Macron amesema ameamua kurejesha chaguo la hatma ya Bunge kupitia kura. Kutokana na hatua uchaguzi utafanyika kwa awamu mbili, Juni 30 na Julai 7.
Hatua hiyo ni baada ya duru kutoka Ufaransa kuonesha chama cha mrengo wa kulia cha National Rally kiko mbele zaidi katika uchaguzi wa Bunge la Umoja wa Ulaya, kuwashinda washirika wa Macron wanaounga mkono Ulaya.
Chanzo: DW