CDF Mkunda awavisha Nishani maafisa na askari

0
222

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda amewavisha nishani maafisa na askari wa vikosi vilivyoko Kanda ya Dar es Salaam na Pwani kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan.

Zoezi hilo limefanyika mkoani Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mgulani leo Juni 07, 2024 kwa kuwavisha Nishani ya Utumishi Uliotukuka Tanzania, Nishani ya Utumishi Mrefu na Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia njema.

Wakati huo huo, Jenerali Mkunda amewavisha Nishani ya Ulinzi wa Amani ya SADC maafisa na askari kwa niaba ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kutambua mchango wao katika ulinzi wa amani nchini Msumbiji chini ya Mwavuli wa SADC iliyowatunuku Nishani hiyo.