Dkt. Biteko: 93% ya uvuvi ni wavuvi wadogo

0
137

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema asilimia 93 ya uvuvi wote hapa nchini unategemea wavuvi wadogo na hivyo ni lazima uwe endelevu kwa manufaa ya sekta nzima.

Akifungua mkutano wa 10 wa wavuvi wadogo Barani Afrika unaofanyika hapa nchini, Dkt. Biteko amesema, bila uvuvi mdogo hakuna viwanda vya samaki wala hakuna samaki kwenye soko.

Ameongeza kuwa takwimu zinaonesha bado sekta ya uvuvi mdogo haijafikiwa vya kutosha na hivyo kutoa wito kwa wadau wote kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa wavuvi wadogo na kuwaendeleza kwa manufaa ya sekta hiyo.

Dkt. Biteko amesema wavuvi wadogo wakiendelezwa basi wavuvi wakubwa watapatikana na hivyo mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa utakuwa mkubwa,

Ametoa wito kwa wadau wote kuangalia namna ya kuwawezesha wavuvi wadogo kwa nyenzo, mitaji, elimu na kuangalia namna ya kupata soko la bidhaa za wavuvi wadogo barani Afrika.