Prof. Shemdoe: Msimamo wa Afrika utapelekwa duniani

0
143

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe amesema msimamo wa wavuvi wa Bara la Afrika utawasilishwa katika mkutano wa dunia kuhusu uvuvi utakaofanyika mwezi Julai mwaka huu Rome, Italia.

Akitoa salamu za wizara hiyo wakati wa Mkutano wa Afrika wa Wavuvi Wadogo unaofanyika Dar esi Salaam, Profesa Shemdoe amesema hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufanyika Barani Afrika na lengo lake ni kujadili na kuona namna ya kuboresha shughuli za wavuvi wadogo.

Amesema mwaka huu ni mwaka wa 10 tangu kufanyika kwa mkutano huo na kwamba utatoa msimamo wa wavuvi wa Afrika kuelekea mkutano wa Dunia wa Uvuvi.

Nchi 32 kutoka barani Afrika zinashiriki mkutano huo ambapo unafunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko.