Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum “Fei Toto” amesema wao kama wachezaji wanatambua ubora wa Yanga Afrika, hivyo wataingia uwanjani kwa kuiheshimu huku akiwataka Yanga nao kuwaheshimu Azam FC.
“Tunawaheshimu sana Yanga SC na wao waje kwa kutuheshimu sisi Azam FC na wakifanya makosa tutawaadhibu.
“Kwa upande wa wachezaji tumejipanga vizuri, hakuna fainali rahisi. Tunawaheshimu sana Yanga, wana wachezaji wazuri, leo tutaenda kufanya mazoezi ya mwisho kufuata zaidi maelekezo ya walimu ili tuone kesho itakuaje,” amesema Zanzibar Finest.
Mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho la CRDB utachezwa kesho katika Uwanja wa Amaan Complex Visiwani Zanzibar. Nini utabiri wako katika mechi hiyo?
Unaweza kupanga ni vikosi gani vitaanza kwa kila timu? Jimwage hapo chini.