JK asisitiza ufadhili sekta ya elimu

0
102

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Ubia wa Elimu Duniani (GPE), ameshiriki katika mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
unaofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Dkt. Kikwete ametumia mkutano huo kuzungumza na vongozi mbalimbali hasa wa kutoka sekta za kifedha, sekta binafsi na washirika wa kimaendeleo kuhusu umuhimu wa kuongeza ufadhili wa fedha ili kuimarisha mpango wa utoaji chakula kwa wanafunzi shuleni.

Pia Dkt. Kikwete ameeleza umuhimu wa washiriki wa mkutano huo kufikiria mbinu mpya za kupata fedha zitakazotumika kugharamia programu za kutoa chakula kwenye shule mbalimbali.

Mkutano huo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika umekuwa ukifanyika kila
mwaka na kuhudhuriwa na Mawaziri wa Fedha na Elimu kutoka nchi mbalimbali duniani, viongozi kutoka Umoja wa Afrika, wawakilishi kutoka AfDB,
wawakilishi wa mashirika ya kimaendeleo pamoja na viongozi wa sekta binafsi kutoka Barani Afrika.