Ubalozi wa Marekani kufungwa leo

0
331

Ofisi za Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania zilizopo mkoani Dar es Salaam, leo Mei 27, 2024 zinafungwa ili kuipa heshima siku ya kuwakumbuka raia wa nchi hiyo waliojitolea kupigania uhuru wa nchi yao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ubalozi huo umeeleza kuwa Rais Joe Biden wa Marekani ametangaza kuwa siku ya leo itumike kama kumbukumbu ya kuwaheshimu wanawake na wanaume majasiri ambao walijitoa mhanga kwa ajili ya Uhuru wa Taifa lao.

Amesema pamoja na kuwakumbuka majasiri hao, Marekani inatimiza wajibu wake wa kuwasaidia walionusurika, walezi wao pamoja na familia zao.