Barabara ya Kiranjeranje – Ruangwa kukarabatiwa

0
166

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Lindi imejipanga kuweka kambi katika eneo labarabara ya Kiranjeranje – Ruangwa ili kuikarabati barabara hiyo iliyoharibiwa na mvua.

Hayo yameelezwa na Meneja wa TANROADS mkoa wa Lindi Mhandisi Emil Zengo alipokuwa akieleza mikakati ya Wakala huo katika urejeshaji wa mawasiliano ya barabara yaliyokatika ndani ya mkoa huo.

Amesema watahakikisha barabara hiyo inapitika katika siku chache zijazo ili kuondoa adha ya usafiri na usafirishaji bidhaa inayowakabili watumiaji wa barabara hiyo ya Kiranjeranje – Ruangwa

Kwa sasa Wananchi wanaotumia barabara hiyo kwa ajili ya usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali, wanalazimika kutumia usafiri wa bodaboda, kwani hakuna gari linaloweza kupita.

Mhandisi Zengo amesema kambi watakayoiweka itakuwa kubwa huku akiiomba Serikali kuwaongeza nguvu ili barabara zote ziweze kupitika muda wote.