NCT na SUZA kushirikiana kupeleka mbele utalii

0
2339

Chuo cha Taifa cha Utalii na Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) kupitia Taasisi ya Utalii vimesaini hati ya makubaliano ya kushirikiana katika kufanya tafiti ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa kuzalisha wataalamu wenye ujuzi katika usimamizi na uandaaji wa matukio kwenye sekta ya utalii.

Wakizunguza mara baada ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Dkt. Florian Mtei na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA), Profesa Mohamed Makame Haji wamesema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za viongozi wa serikali wa pande zote mbili katika kuwavutia wageni wa mataifa mbalimbali duniani kuja kujionea vivutio vya utalii vinavyopatikana nchini na kukuza uchumi wa nchi.

“Tunaamini kupitia ushirikiano huu vyuo vyetu hivi viwili vinaenda kuzalisha watoa huduma walio bora ambao wameaandaliwa na wataalamu wa pande zote mbili na kupata watoa huduma wenye viwango vya kimataifa,” amesema mmoja wa viongozi hao.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mtei amesema katika kuendeleza ushirikiano huo, taasisi hizo zimejipanga pia kuandaa mashindano ya mapishi ya vyakula vya asili ikiwa ni sehemu ya kutangaza utalii wa asili.

@emmanuelsamwel8195 ✍🏽✍🏽🎥