Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Michael Mndolwa amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kusimamia uhuru wa kuabudu na kuonesha msimamo wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Askofu Mkuu Mndolwa ametoa shukrani hizo wakati wa Ibada Kuu ya Upatanisho inayoendelea kwenye Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Zanzibar, Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini.