Serikali kujenga mazingira rafiki kwa Msalaba Mwekundu

0
274

Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Pindi Chana amesema serikali imeendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi kwa Chama cha Msalaba Mwekundu (TRCS) pamoja na kuweka sheria thabiti ili kuhakikisha taasisi hiyo inatoa huduma iliyo bora kwa Watanzania bila ya changamoto zozote.

Aidha amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha serikali inahudumia wananchi wake hasa katika sekta nyeti ya afya maana ndio msingi wa maendeleo ya taifa.

Amesema hayo katika hafla ya maadhimisho ya kitaifa ya miaka 62 ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) kitaifa yanayofanyika jijini Dodoma.