Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ambaye ni mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 62 ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) akikagua mabanda mbalimbali ya maonesho.
Maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa jijini Dodoma ambapo wanachama wa chama hicho kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamehudhuria.
Maadhimisho haya yamebeba kaulimbiu isemayo, “Natoa kwa furaha na furaha ninayotoa ni zawadi.”