Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana ameonesha kuvutiwa kuona makala za video na sauti zilizobeba kumbukumbu ya historia ya Tanzania.
Maktaba hii ipo katika Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zilizopo Barabara ya Nyerere, karibu na Tazara.
Katika maktaba hii zipo kumbukumbu za hotuba za viongozi wote walioongoza taifa la Tanzania. Vilevile zipo kumbukumbu za makala za sauti na video za matukio mbalimbali yakiwemo ya uhuru wa nchi yetu, muungano na Azimio la Arusha ambazo zimebeba historia adhimu ya Tanzania.